HABARI

Fahamu nchi pekee Ulaya ligi yake inaendelea kuchezwa bila hofu ya ‘CORONA’, Messi na Ronaldo waalikwa

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na miamba ya soka ya Hispania timu ya Barcelona, Alexander Hleb amesema kuwa nchini kwao, Belarus hakuna anayejali kuhusu uwepo wa janga la virusi vya Corona na ndiyomaana hata ligi kuu inaendelea kupigwa mpaka sasa.

Image result for Alexander Hleb
Wakati Mataifa mbalimbali yakisimamisha shughuli za michezo ambayo ni chanzo moja wapo cha mkusanyiko wa watu, huku Uefa ikifikiria namna ya kuweka sawa ratiba za msimu lakini nchi hiyo kwao soka lilikuwa likipigwa bila hofu.
Wakati Uturuki Super Ligi ikiwa ya mwisho kusimamisha michezo yake siku ya Alhamisi, taifa hilo la Belarus linalopatikana Mashariki mwa Ulaya bado ligi inaendelea kuchezwa.
“Dunia nzima sasa inaangalia Belarusian league. Kila mtu anakwenda kwenye luninga yake kutuangalia sisi.” Amsema Hleb
 The eastern European nation is the last on the continent still playing
Alexander Hleb ameongeza “Wakati NHL ilipofunga msimu, wachezaji wengi wa ‘ice hockey’ walikwenda Urusi kucheza. Pengine Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanaweza kuja Belarus league kuendelea kucheza huwezi juwa.”
“Ni semehu pekee barani Ulaya unaweza kucheza mpira wa miguu, wala mamlaka hazijawa tayari kusimamisha michezo.”
 Snow oe coronavirus - there is no stopping football in Belarus
Wakati Mataifa ya Ulaya yakizidi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona, Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko kwa upande wake amependeka matrekta ‘tractor therapy’ kutumika viwanjani kama sehemu ya kupambana na virusi vya corona

About the author

kidevu

Leave a Comment