HABARI

Trump ataka Wamarekani wafunguliwe kabla ya Pasaka kunusuru uchumi

Rais Donald Trump amesema anaitaka Marekani “ifunguliwe tena” kabla ya sikukuu ya Pasaka (Aprili 12), licha ya onyo kuwa kufanya hivyo kutaleta hatari kubwa kwa juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo.
Kauli hiyo imekuja kufuatia majimbo 17 ya nchi hiyo kutoa amri kwa wakazi wake kukaa nyumbani kuanzia leo Machi 25, 2020.
Rais Trump amesema Serikali yake itatathmini upya maagizo ya kuepuka mikusanyiko kwa siku 15, yanayolenga kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi, akipendekeza kufuta maagizo hayo mapema wiki ijayo.
Hadi kufikia sasa Marekani imeripoti maambukizi zaidi kwa Watu 55,148 ya virusi vya Covid_19 ambavyo pia vimesababisha vifo vya watu 797.


About the author

kidevu

Leave a Comment