HABARI

Ukaguzi kwa wauza Sanitizer na mask

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa ameagiza Uongozi TBS na FCC kuyafikia maduka yote yanayouza barakoa (Masks) na vitakasa mikono (sanitizers), ili kuweza kujiridhisha na bei za bidhaa hizo kutokana na baadhi ya wamiliki wa maduka kuongeza bei visivyo halali.
“kumekuwepo baadhi ya wafanyabiashara ambao kwa makusudi wamekuwa wakificha Barakoa (face masks), vikinga mkono (gloves), vitakasa-mikono na kemikali za usafi wa mazingira (Hand Sanitizers and Surface Disinfectants) na kupandisha bei kwa nia ya kujipatia faida”
“Huu sio uungwana na ni kukosa uzalendo katika kipindi hiki ambacho kama Taifa tunatakiwa kuwa kitu kimoja. Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara itawafuatilia watu hawa na kuwachukulia hatua”
”Pia tunatarajia kujadiliana na wenye viwanda vinavyotengeneza bidhaa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, au bidhaa ghafi (mf. vileo/alcohol)”

About the author

kidevu

Leave a Comment