HABARI

AZAM FC WATAJA SABABU YA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA NA TANZANIA PRISONS

 


VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa ilikuwa ngumu kupata matokeo mbele ya Tanzania Prisons kwa kuwa ulikuwa ni mchezo wa nguvu nyingi mwanzo mwisho.

Jana, Februari 22 Azam FC ililazimisha sare ya bila kufungana ikiwa ndani ya Azam Complex na kuwafanya wagawane pointi mojamoja kwenye mchezo wa ligi.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela,  Azam FC ilishinda bao 1-0 lilipachikwa na Prince Dube mwenye mabao 7 akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Azam FC.

 Matokeo hayo yanaifanya Azam FC iliyocheza mechi 21 kufikisha jumla ya pointi 37 ikiwa nafasi ya tatu na Prisons ipo nafasi ya 8 na pointi zake ni 26 ikiwa imecheza mechi 20.

Bahati amesema:”Ulikuwa ni mchezo wa kutumia nguvu kubwa mwanzo mwisho jambo ambalo liliwafanya wachezaji wawe kwenye kasi hiyo muda wote.

“Licha ya kutengeneza nafasi ilikuwa ngumu kuzitumia kwa kuwa muda ambao unafika eneo la tukio tayari wapinzani wamefika, kipindi cha kwanza tulianza vizuri ila kipindi cha pili tukaamua kuongeza washambuliaji ili kubadili mbinu ila haikuwa bahati yetu.

“Bado tuna muda wa kufanya maboresho kwenye mechi zetu zijazo na tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” .

About the author

kidevu

Leave a Comment