Header Ads

KISINDA AAMBIWA ASAHAU NAMBA SIMBA, LABDA AWE MWANARIADHA

 

LICHA ya kuwa sababu ya penalti kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliowakutanisha Yanga na Simba, Uwanja wa Mkapa, Tuisila Kisinda ameambiwa hawezi kupata namba ndani ya Simba.

Manara ameongeza kuwa anaamini kuwa kwa namna ambavyo anafanya ndani ya uwanja akiwa mwanariadha kama ilivyo kwa Filbert Bayi anaweza kutusua.

Penalti hiyo ilizua utata ila mwisho wa siku maamuzi ya mwamuzi hayakuweza kuzuiwa.

Kisinda ambaye anacheza Yanga alisababisha penalti baada ya kumzidi spidi beki kisiki wa Simba, Joash Onyango, Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Penalti hiyo ilifungwa na Michael Sarpong ilimshinda mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula na kuiokotea nyavuni.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa anatambua kwamba Kisinda ni mchezaji makini ndani ya Yanga ila hawezi kupata nafasi ndani ya kikosi cha Simba.

"Unazungumza kuhusu Kisinda,(Tuisila) kuja kucheza Simba? Sasa pale atacheza nafasi ya nani maana kila mtu ana namba yake sijui atamchomoa nani kikosi cha kwanza.

"Labda atapendeza akiwa kwenye masuala ya riadha kama akina Bayi,(Filbert) huko anaweza kufanya vizuri ila ndani ya Simba hakuna nafasi kwa kweli na huo ni ukweli kabisa.

"Unapozungumzia Simba unazungumzia timu moja ambayo kupata namba lazima ukomae na uwe bora ndani ya uwanja sasa na wachezaji ambao wanasajiliwa ni lazima wawe imara na bora," amesema.


No comments:

ñ.