Header Ads

MOURINHO:KLABU INA MATATIZO, MBINU NI BORA

 


 JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham Spurs amesema kuwa anadhani timu hiyo ina matatizo na kusifu mbinu zake kuwa ni bora.

Kwa sasa amekuwa kwenye mwendo wa kususua tofauti na awali jambo ambalo linaweka hatari kibarua chake baada ya kurithi mikoba ya Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha PSG.

Februari 21 alishuhudia timu yake ikipoteza mbele ya West Ham United kwa kufungwa mabao 2-1 jambo ambalo limemfanya awe mnyonge kwa kiasi chake.

Kinakuwa ni kichapo cha tano ndani ya Ligi Kuu England kati ya mechi sita ambazo ameongoza kikosi chake ambapo kwenye mchezo huo alishuhudhia mabao ya Michail Antonio na Jesse Lingard na kwa Spurs ilifunga bao lake kupitia kwa Lucas Moura.

Mourinho amesema:"Klabu ina matatizo na siwezi kuyatatua peke yangu,tunapoteza mechi nyingi haya ni matokeo mabaya. Kuhusu mbinu sisi na benchi la ufundi tuna mbinu bora kabisa,".

Spurs imecheza jumla ya mechi 23 kibindoni imekusanya jumla ya pointi 24 ipo nafasi ya 9.

No comments:

ñ.