Header Ads

NYOTA SABA WA YANGA HATIHATI KUUKOSA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO

 

KUELEKEA kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya 32 bora kuna hatihati ya nyota saba wa Yanga kuukosa mchezo huo.

Ikiwa inaongoza Ligi Kuu Bara na pointi zake 49 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 ina kazi ya kuanza kulifukuzia taji la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa Simba.

Februari 27 Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Ken Gold SC saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa nyota ambao wanaweza kukosekana ni pamoja na mshambuliaji wao Yacouba Songne ambaye anasumbuliwa na maumivu ya misuli ambayo aliyapata kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, visiwani Zanzibar.

Abdalah Shaibu,'Ninja' beki wa kati, Ramadhan Kabwili, kipa namba tatu wa Yanga,Tonombe Mukoko alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga hawa wapo fiti na wameanza mazoezi mepesi hivyo ni jukumu la Kocha Mkuu, Cedric Kaze kuamua kuwatumia kwenye mchezo huo.

Wengine ambao bado hawajarejea kwenye ubora ni pamoja na Said Ntibazonkiza, Dickson Job na Balama Mapinduzi,” amesema Naahumu Muganda.

No comments:

ñ.