Header Ads

TONOMBE MUKOKO YUPO FITI KWA AJILI YA MECHI ZIJAZO

 
 UONGOZI wa Yanga umewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu hali ya kiungo wao, Mukoko Tonombe raia wa Congo.

Februari 18, Uwanja wa Mkapa alishindwa kumaliza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kupata majeraha.

  

Kiungo huyo alishindwa kuendelea na mchezo huo uliopigwa baada ya kugongana na mchezaji wa Mtibwa kabla ya kuomba kutolewa.

 

 

Tonombe alitolewa nje katika dakika za nyongeza za mchezo huo akiwa amebebwa na machela.


Ofisa Mhamasishaji wa timu hiyo, Antonio Nugaz, amesema kuwa anaendelea vizuri baada ya kushindwa kuendelea na mchezo huo.

 

 

Nugaz amesema kuwa kiungo huyo anaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu hiyo mara baada ya kutolewa nje.

 

 

Aliongeza kuwa kiungo huyo yupo chini ya uangalizi huku akiendelea kupatiwa matibabu ya haraka ili kuhakikisha anapona haraka na kurejea uwanjani katika michezo ijayo ya ligi na Kombe la FA.

 

 

“Mukoko anaendelea vizuri na kikubwa niwatoe hofu mashabiki wa Yanga juu ya afya yake baada ya jana (juzi) kutolewa nje akiwa amebebwa na machela.

 

 

“Mashabiki wengi walikuwa wakitaka kujua maendeleo yake baada ya kushindwa kuendelea na mchezo, hivyo Tonombe yupo fiti na atakuwepo katika michezo ijayo,” alisema Nugaz.

No comments:

ñ.