HABARI

Mbowe ajiweka Karantini baada ya mtoto wake kuthibitishwa kuwa na Corona “Rais Magufuli alinipigia simu kunipa pole”


Mbowe amesema amejitenga na familia yake ambayo itakuwa karantini kwa wiki mbili, na hivi sasa yupo nyumbani Dodoma akisubiri majibu ya vipimo ili kufahamu kama naye ana Virusi hivyo.
Akiongea na Clouds Media Mbowe amesema tangu aonane na Dudley siku 12 zilizopita, amekutana na watu wengi hivyo ni jambo la kuomba Mungu asikutwe na #CoronaVirus ili aliokutana nao pia wawe salama.
Aidha, Mbowe ameeleza kuwa mkakati wa pamoja unahitajika ili kukabiliana na mlipuko wa Corona ambao amesema ni suala ya kitaifa.
Mbali na hilo Mbowe amethibitisha kuwa Rais Magufuli alimpiga simu na kumpa Pole “Mh. Rais alinipigia simu na kunipa pole”

About the author

kidevu

Leave a Comment