Header Ads

KUMBE WACHEZAJI YANGA WALIKOSA KUJIAMINI


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake awali walikuwa wanashindwa kujiamini jambo mbalo liliwafanya wapate sare mbili mfululizo mzunguko wa pili ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ilianza kukubali sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine kisha ikafuata sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar bao 1-0 na kusepa na pointi tatu na kujikita kileleni ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.

Mtibwa Sugar imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua ambapo kwa sasa ipo nafasi ya 12 ikiwa imekusanya pointi 23 baada ya kucheza mechi 20.

Kaze amesema:"Haikuwa rahisi kupata ushindi kwa kuwa niligundua kwamba wachezaji wangu walikuwa hawajiamini hasa baada ya matokeo mabaya kwetu ndani ya wiki mbili mfulululizo.

"Jambo ambalo nilifanya ilikuwa ni kuzungumza na wachezaji na kuwajengea hali ya kujiamini jambo ambalo limeweza kutupatia matokeo chanya, bado tunaendelea kupambana kwani kazi haijaisha,".

Bao la ushindi Uwanja wa Mkapa lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Carlos Carlinhos dakika ya 72 kwa pasi ya Tuisila Kisinda.

No comments:

ñ.