Header Ads

MANCHESTER UNITED MACHO YOTE KWA FATI

 

MEELEZWA kuwa Klabu ya Manchester United imemtengea pauni milioni 130 nyota wa Barcelona Ansu Fati ili kupata saini yake baada ya dili lake msimu uliopita kuibukia ndani ya Old Trafford kubuma.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 18 yupo kwenye kikosi cha kwanza kwa sasa na anauwezo mkubwa wa kucheka na nyavu jambo ambalo linawapa nguvu United kuipambania saini yake.

Akiwa ndani ya Nou Camp tangu msimu uliopita amefunga jumla ya mabao nane kwenye mechi 33 ambazo alipata nafasi ya kucheza.

Ofa ya mwanzo ndani ya Barcelona ilikataliwa na rais aliyemaliza muda wake ndani ya Barcelona, Josep Bartomeu kwa kile alichoeleza kuwa hawawezi kuacha kipaji hicho kiondoke ila kwa sasa anapewa nafasi kubwa ya kuondoka ndani ya La Liga na kuibukia ndani ya Ligi Kuu England kutokana na timu hiyo kuyumba kiuchumi. 

Hivyo Fanti anapewa nafasi ya kuibuka ndani ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkjaer baada ya kumkosa Jadon Sancho.

No comments:

ñ.